Sira ya Mtume (ya kuisoma) katika dakika chache:
Sifa na vipengele vya kitabu
1. Kijitabu cha kwanza cha mfukonikinachohusu Sira ya
Mtume (S.A.W), ili kiwe pamoja nawe safariniau
nyumbani.
2. Ni Kijitabu kilicho chepesi kukibeba, kidogo, chenye
manufaa mengi, na maana makini.
3. Kijitabu hichi kimekusanya utukufu wa Sira, uzuri wa
mwendowa Mtume (S.A.W), Sunna iliyo safi sana, na
alama za mbinu zake.
4. Matini zake zimechaguliwa miongoni mwa mapokeo
mengi ili kufikia lengo kwa maneno machache.
5. Hakina mapokeo yasiyoaminika wala Hadithi dhaifu,
bali imetolewa kwa makini.
6. Utungaji wake umetegemea Qur‘ani na Hadithi za
Mtume (S.A.W) tu.
7. Kijitabu hichi kinachambua hadhi ya manabii na
heshima zao.
8. Kina maelezo mafupi kuhusu Nabii Ibrahim, Musa, na
Issa (A.S).
9. Kina matukio muhimusana ya Sira yake Mtume
(S.A.W).
6
10. Kina muhtasari wa sifa za Mtume (S.A.W), tabia zake
njema, na dalili za unabii wake.
11. Kina maelezo ya kijumla kuhusu nguzo za Uislamu,
misingi yake, na sheria zake.
12. Kina zaidi ya Aya300 za Qur‘ani na zaidi ya
Hadithi1100 za Mtume (S.A.W) .
13. Kina zaidi ya anuani 500.
14. Kina ufafanuzi wa maneno magumu, maeneo, na
makabila ambayo ni zaidi ya 430.
15. Kina zaidi ya Wahusika (100), na zaidi ya maeneo, na
makabila (200).
16. Kimeandaliwa katika mpangilio wa utaratibu wa
matukio kadiri iwezekanavyo.
17. Kimeandikwa kwa mtindo mwanana wa kifasihi, usio
wa kurefusha au kurudiarudia.
18. Kimeandikwa kwa kufuata kanuni za uandishi
unaokubalika.
19. Kimesomwa, kimepitiwa na kuhaririwa na zaidi ya
wanazuoni,maulamaana nawatafiti 30 waliobobea katika
nyanja hii.
20. Kimefasiriwa kwa zaidi ya lugha 25